-->

Stara Thomas Atoboa Kinachowaharibu Wasanii Wengi wa Kike

Msanii mkongwe wa muziki Stara Thomas ameelezea sababu ya wasanii wengi wa kike wa sasa hivi kuimba nyimbo ambazo hazina maudhui na kupoteza ubora wa muziki, tofauti na ule ambao walikuwa wanafanya kipindi chao.

Akizungumza kwenye kipidi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Stara Thomas amesema wasanii wa sasa hivi wanaimba muziki usio na maudhui wala maadili kutokana na maisha wanayoishi, ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na malezi.

“Unajua mtu anafanya sanaa kutokana na mazingira aliyokulia nini anataka na  nini anachokiona, kwa sababu vile unavyoona ndivyo unavyokua, sasa ukiangalia hawa wasanii mashairi yao wanavyoandika, rudi kwenye historia yao wametokea wapi, hapa lazima kutakuwa na maisha ya aina mbili tofauti” alisema Stara Thomas.

Stara Thomas aliendela kusema kuwa….”Yule anaweza akazungumza masuala ya kukatakata, kwa sababu ya ‘mind set’ yake, mtu anazungumzia ‘party’, mind yake imekaa kiparty, na mwengine huyu akizungumzia kuacha maungo wazi ndiyo mind set yake inavyomtuma na kuna watu wanamuunga mkono, kwa hiyo tunatofautiana na sanaa yetu tunayofanya kutokana na maisha yetu tuliyotoka, mazingira tuliolelewa,”, alisema Stara Thomas.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364