-->

Steps Aanze Kuuza DVD za Kutafsiri Nini Tunachouza?

KAMPUNI kubwa ambayo ilikuwa ndio mahiri katika usambazaji wa filamu Swahilihood ni kampuni ya Steps Entertainment ilitikisa lakini kwa sasa ni kama vile hawapo tena hata lile duka nzuri lilokuwepo mitaa ya Masasi na Mzimbazi likiuza filamu zetu halipo tena bali ni sehemu ya kubeti swali linakuja je waanze kuuza Dvd zilizotafsiriwa kwa Kiswahili?

Wasanii wakiwa katika maandamano kupigania kazi zao.

Ninapokuwa katika daladala hata nikishuka na kukatiza katika mitaa yetu Dvd zinazotamba na kuuza ni zile za nje ambazo zimetafsiriwa kwa Lugha yetu ya Kiswahili wakati sinema zetu zinaigizwa kwa Kiswahili nini kinatufanya tushindwe kuuza kazi zetu?

Nimeshauri Steps ambao ndio wasambazaji wakubwa waanze kusambaza kazi zilizotafsiriwa kwani historia inaonyesha kuwa miaka ya nyuma baada ya soko letu kushikwa na Wanaijeria tuliwatoa sokoni kwa kuwaiga huku tukitumia mtaji wetu wa Lugha ya Kiswahili vizuri kilichotokea wakafa tukakamata soko tukatengeneza Upinzani kati ya The Great na The Greatest.

Wasanii nyota Bongo Ray na Ritchie wakisilikiliza kwa makini.

Bila kuwachosha sana mwisho nauliza wadau Steps aanze kuuza Dvd za kutafsiri kwani tunachouza ni nini katika filamu zetu kama si Lugha yetu tamu ya Kiswahili?!!

 

FilamuCentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364