Steve Nyerere Afungukia Nyumba Ndogo
Komediani wa Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amefungukia tetesi za kuwa na nyumba ndogo akidai kuwa hayo ni maneno ya watu kwani ana mkewe mmoja tu.
Akizungumza na Wikienda , Steve alisema kuwa, watu wanaosema yeye ana nyumba ndogo wanamzushia kwani katika maisha yake hajawahi kuwa na nyumba ndogo.
“Unajua watu wakitaka kukuzushia jambo huwezi kuwazuia, mimi sipendi hata kuzizungumzia hizo ishu, sijawahi na wala sitarajii kuwa na nyumba ndogo,” alisema Steve.
Chanzo:GPL