-->

Steve Nyerere ataka mvutano wa Diamond, Alikiba na Ommy Dimpoz kumalizika

Msanii wa filamu Bongo, Steve Nyerere ametoa ushauri kwa kile kinachoendelea kati ya Diamond Platnumz, Alikiba na Ommy Dimpoz kwenye mitandao ya kijamii.

Wasanii hawa wa Bongo Flava wamekuwa wakitupiana maneno yenye mafumbo katika mitandao ya kijamii tangu Diamond aliposhirikishwa katika remix ya ngoma ya Fid Q ‘Fresh’ ambayo ilitoka hiyo juzi na kudaiwa kuna maishairi ya Diamond yalimlenga Alikiba.

Kupitia mtandao wa Instagram Steve Nyerere amewataka wasanii hao kumaliza tofauti zao kwa kuzingatia hatua ambayo wamefikia kwa sasa hasa pale Ommy Dimpoz alipoweka picha Instagram akiwa na mama mzazi wa Diamond na kuandika ujumbe wenye utata.

NIMEKAA NIMEJIFIKIRIA NIMEONA NISEME KIDOGO, DUNIA MAMA ANA HESHIMA YAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, MAMA NI KIOO CHA FAMILY MAMA NI NGUZO YA FAMILY MAMA NI KIMBILIO LA FAMILY , TUNAWEZA KUKOSEA KOTE LAKINI SI KWA MAMA NDOMANA AMNA LAANA YA BABA ILA LANA YA MAMA IPO NA INAFANYA KAZI HARAKA KULIKO KITU CHOCHOTE, SIZANI KAMA TUNA ELIMISHA JAMII KUPITIA MATUSI YA KUZALILISHA WAZAZI, NYINYI NI KIOO CHA JAMII, LAZIMA MUWE NA KIFUA CHA KUBAKISHA MANENO , MIMI NILIZANI HIZI NGUVU MNAZOTUMIA MNGEWEKEZA KWENYE MZIKI WENU TUNGEFIKA MBALI SANA , MMEJIJENGEA HESHIMA NA MMELITAFUTA JINA KWA SHIDA , ILA MNASAHAU JINA HILO LINAWEZA POTEA KWA SEKUNDE, NAWASHAULI NA NAKUSHAULI WEWE UNAYEZARAU WAZAZI FUTA KAULI NA OMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI ZAKO USUSANI KINA MAMA WOTE AMBAO NAAMINI NI MASHABIKI WAKO NA NDIO WALIOKUFANYA UKAFIKA HAPO, HATUKATAI NYINYI NI BINADAMU INAWEZEKANA MMEPISHANA KAULI ILA KWENYE KUPISHANA WEKENI AKIBA YA MANENO, KUNA KESHO HUJUI ATAKAYE KUSTILI, HAKIKA BUSARA ITUMIKE , YANI NINGEKUWA MIMI NDIO UMEMGUSA RITA WANGU IVO DOOOO, MJINGA HAJIBIWI, KICHAA HAKIMBIZWI , MWIZI SI RAFIKI, NANI KAMA MAMA, ESHIMA ITAWALE ASANTE BY #####UZALENDO KWANZA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364