Kiapo Chamtesa Esha Buhet
Kiapo cha kutochora tena michoro (tattoo) katika mwili wake, alichokitoa msanii wa filamu Bongo, Esha Buhet, kinamtesa baada ya kukikiuka kwa kujichora mkubwa zaidi ya hapo awali. Akizungumza na mwandishi wetu juzikati, Esha alisema alikula kiapo cha kutojichora mwili wake, lakini amelazimika kukivunja baada ya kuamua kumuenzi mama yake mzazi. “Nimefanya hivyo kwa ajili ya mama yangu, nimeona sina sehemu ya kumuweka zaidi ya mgongoni kwangu tena kwa maandishi,” alisema Esha.
Read More..