-->

Tanzanite: Diamond Bado Ananichukia Hadi Leo (Video)

Kukumbusha tu Tanzanite alipata jina miaka kadhaa iliyopita baada ya kuurudia wimbo wa Diamond, Mbagala na kudai ulikuwa wake huku pia baadaye akimtuhumu kumroga. Shutuma hizo zilimkera sana Diamond.
Tanzanite amedai kuwa hadi leo Diamond Platnumz anamchukia.

“Nakutanaga naye [Diamond] lakini si mtu ambaye labda ananipa ushirikiano,” Tanzanite ameiambia Bongo5.

Muimbaji huyo amedai kuwa ugomvi wake na Diamond hadi leo unamwathiri kiasi cha baadhi ya wasanii kukataa kufanya naye kazi.

“Lakini pia kitu ambacho kinanishangaza kwamba dah sijui labda tasnia yetu inaenda wapi, sijui sisi Watanzania tunakuwa na roho gani. Kwasababu ile kitu niliyofanya, inafika time sasa hivi kuna msanii nataka nifanye naye kazi anakataa kwasababu hiyo,” ameeleza.

“Yupo msanii ambaye niliwahi kutaka kushirikiana naye akasema ‘bwana mimi naogopa uligombana na jamaa [Diamond]. Mimi sijafanya kitu kibaya kiukweli. Ukiangalia cover ni vitu ambavyo vinafanyika, sijui kibaya kilikuwa ni nini.”

Tanzanite ameachia wimbo mpya uitwao Usipite akiwa na Dee Pesa.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364