Tausi Mdegela: Sina Mahusiano ya Kimapenzi na Hemed PHD
Muigizaji na mchekeshaji kwenye tasnia ya Bongo Movie, Tausi, amesema hana mahusiano yeyote nje ya kazi na Hemed PHD huku akisema huwa wanakutana kambini na hana hata namba ya simu ya msanii huyo.
Tausi ameibuka na kusema hivyo baada ya kuwepo uvumi wa kujimwaga na staa huyo ambapo aliiambia eNewz “Hemedy ni msanii mwenzangu tu na nilipokuwa nyumbani nilikuwa namuona tu kwenye TV na mara ya kwanza nilipokutanishwa naye na meneja wangu Lamata ilikuwa ngumu hata kuongea naye na nilitetemeka saana na nilikuwa mwoga saana”
Mbali na hilo, Tausi, alizungumza kuhusiana na wavulana ambao wamekuwa wakitamani kuwa naye huku wakijiuliza wataishi vipi na yeye akisema hakuna jambo ambalo haliwezekani kwani hata yeye ana ndoto za kuishi na mwanaume na kuwa na watoto wasiopungua 12.
eatv.tv