-->

TID Ameathirika Kisaikolojia – Q Chief

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Q Chief ameamua kumchana swaiba wake TID kwa kumwambia aachane na tabia ya kuzungumza vitu visivyomuhusu huku akimshauri kwa umri wake ni bora angejitahidi kuangalia jinsi ya kurudi kwenye muziki.

Chief amesema TID ameathirika kisaikolojia kwani kwa hali ya kawaida msanii anayejitambua hawezi kuwa muda mwingi anafuatilia maisha ya mtu mwingine huku akiacha kupambana na hali yake.

“Mimi naona kama watu wazima kila mtu angelia na hali yake na kuangalia jinsi gani anaweza kurudi kwenye sehemu yake, Kwahiyo mimi huwa nachukulia kwanini niwe tatizo kwa mtu mwingine? nahisi kuna kitu special umekiona kwangu na hutaki kuniambia utakuwa unamatatizo. TID anamatatizo ya kisaikolojia hivyo anatakiwa ajitathmini kiundani, kama mpaka waheshimiwa wameamua kukusaidia lazima uoneshe muelekeo ili waendelee kukusaidia”,amesema Q Chief kwenye mahojiano yake na Times FM baada ya kuulizwa chanzo cha kuzinguana na TID mara kwa mara.

Hata hivyo, Q Chief amemshauri TID kwa sasa apiganie zaidi hali yake kuliko kuzungumzia maisha ya watu wengine kwani ni kupoteza muda tu.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364