-->

Fid Q Ajibu Hoja ya Mwakyembe

Msanii Fareed Kubanda ambaye wengi humuita ‘concious rapper’ kutoka bongo, amejibu kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe aliyosema wasanii wasiimbe siasa, na kusema kuwa siyo rahisi kwa wasanii kuacha kitu kitu hicho.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Fid Q amesema Waziri hakuwa sahihi kusema hivyo, kwani siasa ipo kwenye maisha yetu ya kila siku, ambayo wasanii ndiyo kitu ambacho hutazama ili kuweza kufanya kazi zao.

“Nafikiri suala la Waziri wa Habari kusema wasanii wasiimbe siasa halikuwa sahihi, nafikiri labda alitaka asema wasanii wasiwaimbe wanasiasa, kwa sababu siasa ni sehemu ya maisha yetu, na tunaguswa nayo kwa namna moja au nyingine, tunataka au hatutaki, na sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka ili mradi hujavuka mstari, na kazi ya msanii ni kuelimisha jamii si tu kuburudisha”, alisema Fid Q.

Fid Q aliendelea kusema kuwa hata mafanikio ambayo Mh. Waziri aliyazungumzia, anatakiwa atambue kuwa msanii kufanikiwa sio kuwa na mali tu, hata kubadilisha jamii kupitia sanaa yake ni mafanikio makubwa.

“Bob Marley aliimba siasa mpaka leo tunatambua legacy yake inaendelea kuishi, Fela Kuti pia, alafu mafanikio ya msanii siyo lazima masuala ya pesa, magari sijui majumba,  mafanikio kwa msanii ni namna sanaa yake inaweza kubadilisha jamii, na kuamini kwamba pesa, magari  na nyumba za kifahari ndiyo vitu vya mafanikio, si nadharia nzuri na yenye busara kwenye jamii”, alisema Fid Q.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364