-->

TID: Mimi ni Muathirika wa Dawa za Kulevya

Mkali wa bongo Fleva, Khalid Mohamed maarufu kama TID, amekiri kuwa mmoja wa mastaa walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza leo kwenye mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, TID amesema yuko tayari kubadilika.

“Nimekuwa muathirika wa madawa ya kulevya, nimekuja kama kijana aliyepotea njia siku za nyuma. Nilikosea sana familia yangu, mama yangu, marafiki na jamii kwa ujumla, naomba mnisamehe. Niko tayari kuunga mkono vita hii, mnyama nimeamua,” alisema muimbaji huyo.

“Hakuna anayejua nimepitia mangapi hadi kufika hapa, lazima nilihitaji nguvu ya dola. Sometimes in life you can mess tu up, you can try again,” ameongeza.

TID amedai kufahamu kuwa wao watu wataoanza kumhisi kuwa atakuwa ‘snitch’ kwa mkuu wa mkoa na huenda akataja watu wengi, lakini amesema madawa ni janga la umma linalopaswa kupigwa vita.

Amewapongeza Rais Magufuli na Makonda kwa kuwaamsha vijana kuachana na matumizi na biashara hiyo akisema ‘hata serikali ipo tayari kumtokeza shetani huyu’ huyu akiahidi ‘Sitorudi nyuma kamwe.’

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364