TID, Nature, Inspekta Haroun, Adili Kusikika Kwenye Soundtrack ya ‘Karibu Kiumeni’
‘Karibu Kiumeni’ haitarajiwi tu kuja kuwa filamu ya Bongo yenye mafanikio zaidi kuwahi kutokea, bali pia itakuwa filamu ya kwanza iliyokutanisha mastaa wengi zaidi wa Bongo Flava kurekodi original soundtrack yake.
Karibu Kiume ni filamu iliyochezwa na Ernest Napoleon (Going Bongo), Irene Paul, Idris Sultan na mastaa wengine na inatarajiwa kutoka December mwaka huu.
Napoleon ameshare picha Instagram akiwa na waimbaji nguli wa Bongo Flava watakaorekodi soundtrack hiyo inayosimamiwa na P-Funk Majani wa Bongo Records.
“#kiumenimovie all star soundtrack by #pfunkmajani loading #jumanature #inspektaharun #tid #youngkiller #dogojanja #adili #msagasumu #damiansoul,” ameandika Napoleon kwenye picha hiyo.
Wasanii watakaosikika ni pamoja na TID, Inspekta Haroun, Juma Nature, Adili, Young Killer, Msagasumu, Damian Soul na Adili.
Kwenye picha hiyo juu, TID ameandika: We Back in Bussiness Once Again …Long Live MajaNi,Tanzania Need New Sound Fix this Problem
Bongo5