-->

Darasa, Billnas Wamshukuru Mwana FA kwa Kuwatambua

Rapa wawili ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye muziki wa bongo Darasa pamoja na Billnas wamefunguka na kutoa shukrani kwa msanii Mwana FA baada ya msanii huyo kuwatambua na kusema kuwa anawakubali wasanii hao kama wasanii wanaofanya vyema kwa sasa kwenye muziki wa Hip hop.

mwana-fa-1

Mwana FA alisema kuwa Billnas pamoja na Darasa ni wanamuziki ambao wanafanya muziki ambao wao wametaka uwe hivyo na wamepatia kwani wameweza kuufanya muziki wao kutokana na vile wao walitaka kufanya.

Kutokana na kauli hiyo Billnas pamoja na Darasa walikuwa na maneno haya kwa Mwana FA.

“Nafurahi kuona hujawahi kuacha kuni support toka enzi za Lyimo mpaka kuwa Nenga. Tunazima simu fake” alisema Bill Nas

Kwa upande wa Darasa alisema siku zote watu ambao wapo pamoja na wapo real watapeana support hivyo anamshukuru sana Mwana FA kwa kuweza kumtambua na kuonesha anamkubali na kukubali kazi anazofanya.

“Real recognize real no bushit madini yanajuana Mwana FA nimefurahi na naheshima kusikia toka kwako” aliandika Darasa

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364