Tunda Afungukia Picha Tata Zilivyomkosesha Dili
Video queen Tunda amefunguka kuwa picha zilizowahi kuvuja mitandaoni akiwa kitandani na msanii Stan Bakora zilikuwa ni sehemu ya filamu na zilifanya familia yake kuingilia kati na kumkataza kuigiza filamu hiyo ambayo ilikuwa katika maandalizi.
Tunda amevujisha siri hiyo kupitia eNewz ya EATV na kudai kuwa picha hizo zilizomuonesha akiwa kitandani kwenye pozi zenye utata ziliifanya familia yake ishindwe kuvumilia
“Sijawahi kuwa na mahusiano na Stanbakora, yule ni mshkaji wangu wa karibu sana kwa sababu wote tumekuwa pamoja mkoani Morogoro. Zile picha zilikuwa tuna shoot movie lakini zilivyovuja kabla ya movie kutoka wazazi wangu wakaingilia kati na kuzuia ikabidi iishie hapohapo hayakuwa mapenzi bali kazi” Tunda alifunguka.
Aidha mrembo huyo baada ya kukanusha kuwa na mahusiano na Stan Bakora amemtaka aliyekuwa mpenzi wake Young Dar es saalam kuendelea kupambana na muziki wake ili kurudisha jina lake ambalo lilififia baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
“Young Dee ni mtu ambaye namfahamu tulishawahi kuwa na relationship kwa muda mrefu lakini ilishaisha na kwa sasa tumebaki kuwa marafiki ambao tunapiga story za kawaida na kushauriana tu. Nataka kwa sasa akaze tu kwenye muziki kwa sababu ndiyo kitu pekee ambacho kimebaki kitakachomfanya atusue afike mbali na kuhusu madawa kama bado kweli amerudi namshauri aachane nayo japo sidhani kama ni kweli karudi maana nikiwasiliana naye ananiambia hafikirii tena kurudi huko pia amtangulize Mungu kwenye mambo yake” Tunda alimaliza.
Mtazame Tunda katika show hii ya eNewz