Tunda Man Atoa ya Moyoni Kuhusu Babu Tale
Msanii Tunda Man ametoa ya moyoni kuhusu meneja wake Babu Tale ambaye pia anaisimamia Tip Top, kutokuwa karibu nao kama siku za nyuma.
Akizungumza na East Africa Television, Tunda Man amesema ni ukweli usiopingika kuwa Babu Tale haithamini Tip Top kama siku za nyuma, na ni kitendo ambacho kinamuumiza sana msanii huyo.
Pia Tunda Man amesema kitendo cha kutokuwa sawa na Babu Tale ni kitu anachokijutia sana kuwahi kumtokea kwa mwaka 2016.
“Najutia kuwa na misunderstanding na bosi wangu. Kiukweli mimi na bosi wangu Babutale hatuko sawa, kosa silijui. Kuna kitu mimi nimemkosea may be au ameamua tu kukasirika na kiukweli hii kuwa mbali na bosi wangu kwenye kazi zangu ninazozifanya nakuwa mwenyewe tu kiukweli it’s pain, naumia.”
“Lakini sometimes mtu anaweza akawa na mwanae akamwambia nenda katafute maisha kivyake japo baba yake anakila kitu, kwahiyo unakuta mtoto anaondoka kutafuta maisha mengine, anabeba zege anafanyaje lakini anajutia kuwa mbali na baba yake. Lakini mimi najutia kwa sababu kazi zangu nakuwa na wakati mgumu wa kuzipush na kusupport kazi zangu lakini Alhamdulillah Mungu anasaidia.”
Tunda ameongeza kuwa kuna kipindi alipata dili la kufanya tangazo lakini kuna mtu alimpandia na nafasi hiyo akapewa msanii mwingine anayesimamiwa na Tale.