Picha: Alikiba Ashiriki Kwenye Mechi ya Soka ya Hisani Uganda, Atunukiwa Tuzo
Kama isingekuwa muziki, huenda Alikiba angekuwa mmoja wa vinara wa timu kubwa za soka nchini, zikiwemo Simba au Yanga.
Pamoja na kufanya muziki, Alikiba hutumia muda wake mwingine kujikumbushia kipaji chake cha soka, na ndio maana Jumamosi hii alishiriki mechi ya hisani ya mchezo huo jijini Kampala, iliyopewa jina ‘A Celebrity For Charity.’ Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Kabira Country Club na kuhusisha nyota wengine akiwemo Emmanuel Okwi.
Timu ya Alikiba na Okwi ilishinda mabao 4-1 huku Kiba akifunga bao la 2.
“We won the game!!! White KingKiba team 4 The Green Team 1
Second goal courtesy of your King. Thank you Uganda for the Award for Best Celebrity Player Award,” ameandika Alikiba kwenye Instagram.
Bongo5