-->

Tunda: Mwanaume Niliyetamani Kuwa Naye Si Young D

VIDEO queen matata Bongo, Tunda Sebasita ‘Tunda’ hivi karibuni ameibuka na kumkana aliyewahi kuwa mpenzi wake David Ganzi ‘Young D’ kuwa si mwanaume hasa aliyewahi kutamani kuwa naye huko nyuma na juu ya uhusiano wao ni jambo ambalo lilitokea tu.

Tunda na Young D

Akichonga na Uwazi Showbiz, baada ya kuulizwa ni mwanaume gani alitamani kuwa naye Bongo huko nyuma na hakupata bahati ya kuwa naye, Tunda alisema hayupo maana mwanaume aliyetamani kuwa naye amekwisha kuwanaye lakini si Young D.

“Siwezi kulitaja jina lake wazi, lakini kiukweli mwanaume ambaye nilitamani sana kuwa naye tayari nilikwishakuwanaye na tukaachana lakini naweka wazi kuwa si Young D,” alimaliza Tunda.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364