-->

Kesi ya Wema Sepetu Kusikilizwa Juni Mosi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi ya kukutwa na bangi inayomkabili Muigizaji maarufu, Wema Sepetu na wenzake umekamilika.

Hatua hiyo imefikiwa leo  ambapo upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kwamba upelelezi umekamilika dhidi ya msanii huyo na wakili wa Serikali Helleni Mushi ameomba kesi hiyo kuarishwa leo na kupangwa tarehe ya kuanza kusikilizwa ili watuhumiwa waanze kusomewa maelezo ya awali.

Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. Mbali na Wema washitakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abas (16), ambapo wote wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4 mwaka huu, nyumbani kwao Kunduchi Ununio , Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.

Hakimu Simba amesema  kesi hiyo itaanza kusikilizwa, Juni Mosi, mwaka kwa watuhumiwa kuanza kusomewa maelezo ya awali.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364