-->

Tuzo Zimeleta Faraja Kwenye Filamu – Gabo

Msanii wa filamu ambaye kwa sasa ndiye ‘hot cake’ kwenye tasnia, Gabo Zigamba, amesema wasanii wa filamu wamepata kwa faraja kuanzishwa kwa EATV AWARDS.

gambo02

Akizungumza na EATV Gabo amesema kwanza ni changamoto kubwa kwao kwani itatengeneza ushindani, ukizingatia kwa upande wa filamu kwa muda mrefu kumekuwa hakuna kitu cha kuwafariji  na kutambua mchango wa wasanii wa filamu.

“Kwangu naichukulia kama changamoto kubwa sana, kwa sababu kwenye industry ya movie hakuna tuzo za namna kama hiyo, wenzetu wana tuzo nyingi ndiyo maana inaonekana kama kwao kunaenda mbele kwetu kuna drop, kwa hiyo tuzo ya East Afrika ambayo wameileta, kwangu mimi naichukulia kama kitu fulani ambacho ni faraja na kitatengeneza competition, inaweza ikaanza taratibu lakini kesho na kesho kutwa inaweza ikashika hatamu”, alisema Gabo.

Pia Gabo alisema yeye binafsi ameshiriki kwenye tuzo hizo na ana imani ndiye mtu wa kwanza kuleta fomu baada ya kusikia tu kuhus tuzo.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364