-->

Usiwaze Kunifikia Utakuwa Mtumwa Wangu – Diamond

Msanii Diamond Platnumz amefunguka na kuwataka wasanii ambao wanachipukia na wale ambao wapo kwenye muziki wafikiri kufanya mambo zaidi yake na wasifikirie au kuwaza kuwa kama Diamond Platnumz.

Diamond843

Diamond Platnumz alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusema wasanii ambao watakuwa wakimuwaza yeye watakuwa watumwa wake, lakini kama watafikiria kufanya vitu zaidi yake itasaidia kwani itafanya kila mtu kuwa na njia yake na kuweza kufanikiwa zaidi katika muziki wao pamoja na maisha kiujumla.

“Mimi nataka kuwaambia wasanii wafikirie kufanya vitu vikubwa zaidi wasifikirie kuwa kama Diamond Platnumz, maana kama watakuwa wanafikiria kuwa kama mimi watakuwa watumwa wa muziki wangu na maisha yangu, mfano unafikiri Wizkid angeamua wa ‘copy’ P Square ingekuwaje? Jibu angekuwa mtumwa wa P Square lakini kwa kuwa alitoka kivyake vyake ndiyo maana saizi Wizkid anafanya vizuri zaidi hata ya P Square ulimwenguni” alisema Diamond Platnumz.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364