-->

Mzee Yusuph Ameacha Muziki na Kumrudia Mungu

Mfalme wa muziki wa taarabu mzee Yusuph maarufu kama “mfalme wa taarabu” amefunguka na kusema kuwa sasa ameamua kuachana na muziki huo na kumrudia Mungu huku akiwataka watanzania pia kumrudia Mungu.

Mzee

Mzee Yusuph akiwa ana swali nyumbani kwake.

Akiongea na eNewz baada ya kutoka msikitini Mzee Yusuph amesema kwa taarifa za awali watanzania wanatakiwa kutambua kuwa yeye ameachana na muziki na sasa amemrudia Mungu na kuwataka kuwa na subira kwani atatafuta siku maalum yeye kutangaza suala hilo ambapo atafunguka kwa kirefu zaidi kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo.

“Ni kweli nimeamua kuachana na muziki na sasa nimemrudia Mungu, nawaomba watanzania wengine pia wamrudie Mungu, nitatafuta siku ambayo nitaongea kwa kirefu zaidi juu ya suala hili, hivyo watanzania watambue tu nimeachana na muziki sasa” alisema Mzee Yusuph.

Hii ni mara ya pili kwa mzee Yusuph kutangaza kuacha muziki kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka jana, alitangaza kuacha muziki na kuingia kwenye siasa lakini hakuweza kufanya vizuri kwenye siasa na kurudi tena kwenye muziki.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364