-->

Uwoya: Huu Ndiyo Ukweli wa Mimi na Ndiku

DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya aliyekuwa mume wa ndoa wa muigizaji nyota, Irene Uwoya aitwaye Hamad Ndikumana kutema povu kubwa katika mitandao ya kijamii, akimsema vibaya mzazi mwenzake huyo, mrembo huyo naye ameibuka na kuanika kile alichodai, ni ukweli kuhusu wawili hao, Risasi Mchanganyiko linaripoti.

HUYU HAPA IRENE UWOYA

Risasi Mchanganyiko lilifanya jitihada za kumfikia muigizaji huyo mwenye umbo la kupendeza na kutaka kufahamu machache kuhusiana na mgogoro huo wa wanandoa ambao umedumu kwa muda mrefu sasa. “Huyu mwanaume ni wa ajabu sana, sijui hata niseme nini, hapa ninapozungumza na wewe hata shilingi moja ya Ndikumana ya kumlea mwanaye siijui, kitu kilichosababisha ndoa kuvunjika yeye anakifahamu ndiyo maana haweki wazi.

“Kila siku anasema kuhusu kunipa talaka, sasa kwa nini asisaini na kunipa ili kila mtu awe na maisha yake, mimi siwezi tena kuwa naye, nasubiri mwanaume mwingine anioe, cha msingi yeye asaini talaka anipatie.

VIPI KUHUSU MADAI YA KUMBANIA MTOTO?

“Mtoto Krish ni wake na hiyo itabakia kuwa hivyo siku zote, sijawahi kumzuia kumsalimia mwanaye, ili iweje, lakini muulize yeye anampatia matunzo? Maana siyo sawa mtu kudai haki bila kutimiza wajibu wako. Huyu mtoto ni wa Ndikumana, kila mtu anajua na itabaki hivyo daima.

NI KWELI KUHUSU DOGO JANJA?

“Jamani mambo mengine hebu hata tuwe na subira basi, yaani mimi yule mtoto mdogo vile ninampeleka wapi? Sitaki kuzungumzia hizo habari kwa sasa.

IRENE UWOYA AMEBADILIKA?

“Yes, mimi siyo Irene yule unayemfahamu, huyu wa sasa ni mwanamke anayejituma, anayetafuta maisha yake mwenyewe, siyo mtu wa kutegemea kuendesha maisha kwa pochi ya mtu. “Ninapambana na hali yangu na nashukuru Mungu kwamba mambo yanaenda, mimi na mtoto wangu tunalala na kuamka vizuri, ujumbe ni mmoja tu kwa Ndikumana, asaini talaka yangu na anipe, mimi siwezi tena kuwa mke wake,” alihitimisha muigizaji huyo.

ALICHOKISEMA NDIKUMANA

Mwanasoka huyo raia wa Rwanda, alisema yupo tayari kumpa talaka mkewe huyo wa zamani, ili aendelee na maisha yake maana amechoshwa na skendo chafu za mara kwa mara kwa mwanamke huyo muigizaji. Katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Ndikumana alisema amekubali kumpa Irene talaka, hivyo asisubiri hadi afe ili aolewe, ili ampe uhuru anaouhitaji aweze kufanya mambo yake bila yeye kuhusishwa.

“Ulilia muda kwamba unataka talaka ili uolewe, sina kipingamizi tafuta kila utakacho ulete nitakusainia, usisubiri nife ili uolewe maana naweza kuishi zaidi ya unavyofikiria, Mungu akusimamie,” aliandika Ndikumana huku akilalamika kuwa Uwoya ameshindwa kumpa nafasi ya kuzungumza na mtoto wake waliyezaa pamoja.

TUJIKUMBUSHE

Mastaa hao wawili, mwanasoka huyo wa zamani wa Rayon Sports ya nyumbani kwao Rwanda na Uwoya, walifunga ndoa mwaka 2009 na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume kabla ya kutengana mwaka 2011.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364