Uwoya: Kuzaa Walizwe Wasio na Watoto
STAA mwenye mvuto wa kipekee wa Bongo Muvi, Irene Uwoya amefunguka kuwa anachukizwa na ishu ya kuulizwa lini ataongeza mototo mwingine baada ya mtoto wake wa kwanza, Krish huku kukiwa na mastaa wengine ambao hawana hata mtoto wa kusingiziwa.
Akizungumza na 3 Tamu, Uwoya alisema kuwa, hata kama yeye hatazaa tena, lakini ishu hiyo haita msumbua kwa sababu tayari Mungu, amembariki hivyo jambo la yeye kutoongeza mtoto mwingine halimuhusu kabisa.
“ Nashangaa sana mtu anakwambia Krish amekua mkubwa anahitaji mdogo wake, ni jambo la kushangaza kwa sababu ambao kuna mastaa wengine umri unayoyoma lakini hawana hata mtoto wa kusingiziwa,” alisema Uwoya.
Chanzo:GPL