-->

Vanessa mdee Auza Nakala 750 za CD ya Money Mondays Mlimani City

Msanii wa muziki Vanessa Mdee amesema ameuza nakala 750 za CD ya albamu yake ya Money Mondays, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MCL Digital, Vanessa amesema nakala hizo aliziuza Jumamosi Januari 20,2018 siku ambayo pia alikutana na mashabiki wake.

Amesema, “Nilipofikia ni msanii wa kimataifa, hivyo lazima nifanye mambo kuendana na wenzangu wanavyofanya, bila kujali nitapata hasara au la.”

Katika uzinduzi huo watu mbalimbali walijitokeza ambao baadhi walinunua nakala za CD hiyo na wengine walipiga naye picha.

Nakala ya albamu hiyo yenye nyimbo 17 aliiuza Sh10,000 kila moja. Ndani yake yamo mashairi ya kila wimbo.

Image result for vanessa mdee selling her monday money cds

Full: Money Monday Album Listening Party ya Vanessa Mdee

Comments

comments

Post Tagged with , , ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364