-->

Victor Wanyama Apewa Mtaa Ubungo – Dar

Meya wa Manispaa ya Ubongo Boniface Jacob, amemtunuku mtaa, Kiungo wa Tottenham ya England Victor Wanyama raia wa Kenya.

Jacob ambaye ni Meya akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameonekana kufurahishwa na mchezaji huyo kufika katika eneo lake na kuunga mkono michezo.

Hivyo kwa kufurahishwa na namna alichofanya kiungo huyo Mkenya ambaye ni nahodha wa Harambee Stars ameamua kumzawadia Barabara.

Wanyama amepewa jina la mtaa uliyokuwa katika mtaa uliokuwa ukifahamika kwa jina la  Viwandani.

Kabla, Wanyama alihudhuria mashindano ya Ndondo Cup yanayoendelea katika Uwanja wa Kinesi Ubungo Shekilango jijini Dar es Salaam jioni hii.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364