-->

Young Killer Amjibu Nay wa Mitego

Baada ya rapa Nay wa Mitego kumchana Young Killer kwenye ngoma yake mpya ‘Moto’ kuwa dogo sasa chali na safari yake kurudi Mwanza inanukia kutokana na msanii huyo kuonekana kupotea kwenye muziki kwa kile anachodai kuwa aliwadharau waliomtoa.

Kufuatia diss hiyo Young Killer ameamua kujibu mapigo kwa Nay wa Mitego na kusema kuwa mara kadhaa ameshakutana na Nay wa Mitego na alikuwa akimpa ushauri mbalimbali juu ya kazi ya muziki na kusema hata yeye sasa atampa zawadi yake ya Eid Mubarak na anaamini ataisikia na ataipenda.

“Katika watu wote sidhani kama mimi ni msanii ambaye nimepotea sana lakini nadhani Nay wa Mitego amesema hivi kwa kuwa ameona kwenye ngoma yangu niliwachana watu, kwa hiyo katika kuniweka sawa mimi naona na yeye hayuko sawa hivyo sina budi kumuweka sawa pia kulingana na utamaduni wangu brother Nay wa Mitego nitakupa zawadi ya Eid Mubarak siku mbili hizi na naamini utapambana na hali yako na utaenjoy kile utakachokisikia baba” alisema Young Killer

Mbali na hilo Young Killer amethibitisha kufanya kazi na msanii Harmonize na kusema muda wowote kazi hiyo itatoka na kusema kuwa Harmonise ameitendea haki sana kazi hiyo.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364