-->

VIDEO: Alikiba ana Roho Ngumu – Hussein Machozi

Hussein Machozi amesema ‘team’ katika muziki wa bongo fleva zimekuwa nzuri kwani zinafanya mashabiki waendelee kukomaa na msanii wao ila anasema yeye hawezi kwani hana roho ngumu kama Alikiba ambaye anatukanwa na watu mitandaoni na kukaa kimya.

Hussein Machozi amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha eNewz na kusema yeye mtu akimtukana kwenye mitandao ya kijamii anaumia sana na lazima amtafute ili amfundishe adabu anasema yeye hawezi kuwa na uvumilivu waliokuwa nao wakina Alikiba na wasanii wengine ambao wana team hizo kwenye mitandao.

Mtazame hapa Hussein Machozi akifunguka zaidi.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364