-->

Video: Baada ya Kuitwa Nyani, Hamorapa Atoa Maneno Mazito kwa Iyobo

DANSA mashuhuri kutoka lebo kubwa Bongo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye pia ni mzazi mwenza wa Anti Ezekiel, Mose Iyobo, amefunguka kupitia mtandao wa ‘Tweeter’ wa  Hamis Mandi Mtangazaji wa XXL ya Clouds FM baada ya Bdozen ‘Hamis’ kuweka picha akiwa na mtafiti wa wa Nyani (Sokwe) duniani, Jane Goodall, ambapo (Iyobo) alimtaka mtafiti huyo apewe taarifa za uwepo wa nyani mwingine aitwaye Harmorapa.

“Duh, noma sana ila mwambie kuna nyani anaitwa Harmolapa,  angekuja kumfanyia utafiti na kujua tabia zake angetisha sana,” aliandika Mose Iyobo miongoni mwa Tweets za post hiyo.

Haijafahamika sababu ya Iyobo kumuita hivyo Harmorapa jina la mnyama, kitendo kinachotafsiriwa kama ni dharau au huenda ipo tofauti kati yao.

Global Publishers imempata Harmorapa na kutaka kujua kauli yake kuhusu maneno hayo ambapo amefunguka maneno mazito, msikilizi mwenyewe kwenye kipande cha video hii hapo chini:.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364