-->

VIDEO: Fid Q Asimulia Enzi za Zamani za Bongo Records

Miaka ya nyuma, Bongo Records kwa Tanzania ilikuwa label ambayo msanii akiwa chini yake alikuwa akionekana kama mfalme, kwa mujibu wa Fid Q.

Fid Q

Hakikuwa kitu cha mzaha kumridhisha P-Funk Majani hadi akuweke kwenye roaster ya wasanii wake. Akizungumza na Lil Ommy wa Times FM kwenye kipindi cha The Playlist, Fid alielezea mashavu waliyokuwa wakiyapata wasanii wa Bongo Records mtaani.

“Enzi hizo ukiwa upo Bongo Records mtaani kwako unaheshimika, unakutana na washkaji wanakupa ofa za bia, maskani una siti yako maalum ‘mshkaji yuko Bongo Records’ hujatoa hata ngoma hata moja! Yaani watu wanakuangalia kwa adabu ‘oyaa jamaa yupo Bongo Records anafanya album yule, noma wewe.’ Ndio Bongo Records ilikuwa iko hivyo.”

Tazama interview nzima hapo juu.

Bongo5

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364