-->

VIDEO: TID ni Paka – Steve Nyerere

Msanii wa vichekesho Steve Nyerere ameibuka na kumjibu msanii TID huku akieleza kufurahishwa na hatua ya TID kumfananisha na panya kwa kuwa inaonesha jinsi alivyo mjanja ambaye anaweza kujitafutia na kusema

Wakati akifurahi kufananishwa na panya, Steve amemfananisha TID na paka ambaye husubiri kutengewa kila kitu.

Steve Nyerere alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kudai kuwa kubishana naye ni kupoteza muda na kwamba yeye ana majukumu mengi yanamtegemea tofauti na TID ambaye hana chochote cha kupoteza.

“Mimi siwezi kubishana nae kwa sababu hata ukituangalia mimi na yeye ni kama vidole na ndio maana havifanani yeye wakati wake umekwishapita na sasa ni wakati wangu lazima ajenge heshima. Nyuma yangu nina familia ambayo inanitegemea, ninalipa kodi,mafundi tofauti na yeye ambaye anaka nyumbani”. Amesema Steve

Steve akaendelea kusema….

“Panya ni mjanja sana akifanikiwa kuingia ndani hautakaa ndani na mkeo kwa amani, afadhali ya mimi panya mjanja kuliko yeye paka ambaye anasubiri kutengewa ale tu”

Akizungumzia suala la kwenda mahakamani kwa ajili ya sauti yake kusikika akimshutumu TID kupokea fedha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuwa kimvuli kwenye sekeseke la watu wanaotumia madawa ya kulevya Steve amemuomba radhi TID na kuongeza kuwa kama atataka wafike atakubaliana naye kwa sababu ni chombo cha sheria.

“Kama yeye ameliona hilo basi niko tayari, lakini sihitaji kufika huko, natumia nafasi hii kwa yeye mwenyewe huko alipo kama nilimuudhi kwa maneno yale ya mama  naomba samahani kwani mimi ni binadamu na binadamu huwezi fanya yote mazuri mimi, na panya huyu naomba msamaha kwako paka, pia naomba ukiona gari langu uendelee kulikimbiza japo elfu kumi, elfu tano napenda sana”. Amesema Steve

Tazama video hii kupata majibizano ya TID na Steve Nyerere.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364