-->

VIDEO: Harmorapa Afunguka Mapya Penzi la Wema, Adai Kuonja Penzi la Amber Lulu

RAPA anayekuja kwa kasi Bongo, Harmorapa amefanya intavyuu na Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho cha Couds FM, Diva The Bause, ambapo rapa huyo amefunguka mambo kibao ikiwemo ishu ya kudai kuwa anampenda Malkia wa Bongo Movies, Wema Sepetu.

Miongoni mwa mambo aliyoyafungukia, Harmorapa ameeleza ukweli kuhusu ishu iliyovuma miezi michache iliyopita, pale alipojinadi kwamba anampenda sana Wema Sepetu na yupo tayari kufunga naye ndoa, ambapo Wema alicharuka na kumjia juu.

Ameeleza ukweli wa ishu nzima na kama amewahi kuwa kwenye penzi la Wema au Laa. Pia amesema siyo kweli kwamba yeye anapenda kiki bali kiki ndiyo huwa zinamfuata. Akitolea mfano ishu ya kutolewa bastola kwa Nape Nnauye, Harmorapa amesema kwamba alikuwa kwenye harakati zake akielekea kwenye intavyuu kwenye redio moja Bongo ambapo alipofika Namanga ndipo alipokutana na sakata hilo lililosababisha atoke nduki kali.

Kuhusu ishu ya yeye kudaiwa kutoka na Amber Lulu kimapenzi ambapo kwa sasa wameshaachana kutokana na kutofautiana naye.

Pia ameeleza tofauti iliyopo kati yake na Harmonize japo wanatoka mkoa mmoja wa Mtwara huku akianika mkali wa Bongo Fleva anayemkubalia na yuko tayari kufanya naye kolabo kati ya Diamond na Ali Kiba.

 

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364