-->

VIDEO: Singeli Tupunguze Maneno Machafu- Man Fongo

Msanii  Man Fongo amewataka wasanii wenzake wa kisingeli nchini kupunguza ukali wa maneno katika tungo zao wanazozitumia kwenye kuimba kwa madai muziki huo ndiyo pekee wa asili uliyobakia katika kulitangaza taifa kwenye soko la kimataifa

Man Fongo amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz cha EATV huku akisisitiza kuwa muziki huo unasikilizwa na watu wa rika lote hivyo ni vizuri kwa wasanii kutumia mafumbo sehemu zenye matusi ili mtu awe na kazi ya ziada ya kulifumbua neno hilo lilikuwa linamaanisha jambo gani.

“Tupunguze kidogo ukali wa maneno kwa sababu ukiweka ukali wa maneno zaidi inawafanya watu wanashindwa kutuelewa kutokana sasa hivi muziki wetu umeshakuwa mkubwa unaeleweka na wakina mama, watoto wadogo pamoja na watu wazima…Tunataka tupambane tuzidi kufika kimataifa zaidi, asiwe anatoka Man Fongo tu leo kaenda huku basi kesho tumsikie mwengine kama Shoromwamba au nani.. Wote tutoke tupige muziki wetu tukautangaze….Tutoe ule ukali wa maneno kidogo, nikisema ukali wa maneno nina maanisha tutoe yale matusi kwa maana ukiongea kwa moja kwa moja utakuwa ujafumba inabidi ufumbe uweke katika mafumbo kidogo mtu awe na kazi ya kulifumbua lile neno”. Alisema Man Fongo

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364