Video: Hussein Machozi Arudi Bongo
Msanii wa muziki, Hussein Machozi, Jumatano hii usiku aliwasili jijini Dar es salaam katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea nchini Italy alipokuwa katika shughuli zake za masomo na muziki.
Muimbaji huyo ametua nchini akiwa na video yake mpya iliyoandaliwa nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mchache baada ya kuwasili, Hussein amedai amejifunza vitu vingi nchini Italy ambavyo amekuja kuvifanya nchini kwaajili ya kustawisha muziki wake.
“Namshukuru Mungu safari yangu imekuwa na mafanikio makubwa sana, masomo yanaendelea vizuri kwa sababu ndio kitu kilichonipeleka,” alisema Hussein. “Nimekuja na audio ya wimbo mpya pamoja na video ambayo imeandaliwa kule na ni kazi nzuri sana ambayo itapendwa na mashabiki wangu,”
Muimbaji huyo amedai amekuja nchini kwaajili ya kuachia kazi zake mpya za muziki na baada ya hapo atarejea Italy kwaajili ya kuendelea na masomo.