-->

Natamani Kufanya Kazi na Chid Benz-Ray C

Msanii mkongwe ambaye kwa sasa anasikika na ngoma ya ‘Unanimaliza’  Rehema Chalamila ‘Ray C’ amekiri kutamani kufanya kazi nyingine na rapa Chid Benzi na anamuombea kwa Mungu ili aweze kutoka rasmi kwenye mtihani wa dawa za kulevya

Ray C amefunguka hayo hivi karibuni na kusema kuwa mbali na kuwa walisha fanya wimbo wa pamoja na Chid Benz kipindi cha nyuma wa ‘Nihurumie’ bado uwezo  mkubwa wa kimuziki alionao Chid ni sababu inayompa shahuku kubwa ya kutaka kufanya naye kazi kwa mara nyingine.

Chid benzi ni bonge la msanii na kwa upande wa Hip hop nadhani ni ‘one of the best artist’ na kwa sasa hayupo pengo lake linaonekana. Nampenda sana Chid Benzi  na ninamuombea sana kwa Mungu aweze kutoka katika janga hilo la madawa na akirudi natamani kufanya nae kazi nyingine. Aweke nia naamini atatoka” alisema Ray C

Pamoja na hao Ray C ametoa ushauri kwa watu wanaopitia matatizo haswa utumiaji wa madawa za kulevya na kusema kama ukitanguliza nia ya kuachana na mateso lazima utashinda mitihani.

Binadamu wote lazima wapitie mitihani lakini tatizo mitihani hiyo lazima itakuwa inatofautiana. Haifurahishi kabisa kumuona mtu anateseka na matumizi ya dawa .Kama binadamu lazima uwe na nafasi ya kujifikiria kwa sababu hakuna mtu anayeweza kubebea ugonjwa au matatizo. Naamini Mungu aliyenisaidia mimi nikatoka kule atawasaidia wote siyo Chidi tuu bali wote wenye nia ya kuachana na yale mateso”– aliongeza Ray C.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364