-->

VIDEO: Jay Moe Amkana T-Touch

Msanii wa mkongwe wa ‘ hip hop’ mwenye hit ya ‘Nisaidie kushare’ Jay Moe amefunguka kwa kusema hawezi kusainiwa na mtu yoyote yule akidai yeye mwenyewe ana label yake ya So Famous na kuna wasanii wanamtegemea.

Jay Moe amefafanua hayo baada ya kuenea tetesi zilizokuwa zikiwaaminisha watu kuwa huenda akasainiwa na Mr T-Touch ili aendelee kutoa nyimbo chini ya uongozi wa ‘Producer’ huyo.

“Mimi ni C.E.O wa so Famous entertainment kwa hiyo siwezi kusainiwa na mtu mwingine wakati mimi mwenyewe nataka kusaini watu, mimi sipo kwa T-Touch wala sipo tayari kusainiwa na ‘record label’ yoyote kwa sababu nina label nataka niikuze nisaidie wengine ambao wapo nyuma yangu, wanataka waone mafanikio yangu ili na wao yawanufaishe” – alisema Jay Moe

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364