Johari Apata Pigo
DAR ES SALAAM: Pole! Staa wa kitambo wa sinema za Kibongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ amepata pigo ‘hevi’ baada ya kufiwa na shangazi yake aliyemlea tangu akiwa mtoto, kumsomesha na kumfundisha maisha hivyo kuondoka kwake kumemuachia maumivu na pigo kubwa.
Johari, akiwa nyumbani kwao mkoani Shinyanga kuhudhuria msiba huo aliliambia Wikienda kwa njia ya simu kuwa, aliumia mno alipopata taarifa za kifo cha shangazi yake huyo aliyekuwa nguzo muhimu maishani mwake.
“Nimekuja Shinyanga kumzika shangazi yangu, tumeshamzika, lakini kwa kweli ameniacha mpweke sana maana ndiye aliyenilea, kunisomesha na kunifundisha maisha, kiukweli ni pigo kwangu,” alisema Johari.
Chanzo:GPL