VIDEO: Mh. Temba Alizwa Mali Zake
Msanii Temba kutoka TMK Wanaume amefunguka na kuweza wazi kuwa alikwama katika muziki na kushindwa kuachia kazi zake mwenyewe baada ya kutapeliwa pesa zake na mtu ambaye alikuwa akifanya naye biashara za magari.
Mh. Temba alisema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live na kudai kuwa alimuamini sana Mustafa lakini hakujua kuwa alikuwa anatengenezwa ili aje kupigwa pesa zake.