VIDEO: Msiniite Tena TID-Khalid
Mkongwe wa bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID au Mzee Kigogo amelikataa rasmi jina la TID ambalo ndilo lililompatia umaarufu na kutaka kupendekeza aitwe jina lake alilopatiwa na wazazi wake au ‘Mnyama’.
Akipiga story na eNewz ya EATV TID amesema halipendi tena jina hilo kwa kuwa limekuwa la kawaida sana na kudai watu waliopo mikoani ndiyo wanapaswa kulitumia na waliopo Dar es salaam wamuite Mnyama au Khalid.
“Sitaki watu waniite TID, niite Mnyama nikiwa mtaani mimi ni Khalid, jukwaani ndiyo TID. Tatizo jina la Top In Dar limekuwa too casual sana mpaka nachukia. tuwaachie watu wa kikoani huko ndiyo waniite TID lakin wa hapa mjini we ukinisalimia niite tu Khalid inatosha” alisema TID
Hata hivyo msanii huyo hakufafanua kwa undani kwanini hapendi kuitwa jina hilo licha ya kuwa ndilo lililompatia umaarufu kabla ya kupata majina tofauti tofauti kama Mzee Warioba, Mzee Kigogo, Mnyama na mengineyo.
Mtazame hapa