-->

VIDEO: Nay wa Mitego Akutana na Waziri Mwakyembe Dodoma

Staa wa Bongofleva Nay wa Mitego alifika katika ofisi za Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na michezo zilizopo Dodoma kwa ajili ya kuonana na kufanya mazungumzo na Waziri Dr. Harrison Mwakyembe ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu msanii huyo kuachiwa huru.

Nay wa Mitego na Waziri Dr. Harrison Mwakyembe

Nay wa Mitego alikuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi Dar es slaam kwa tuhuma za wimbo wake wa ‘WAPO’ kudaiwa kutokuwa na maadili kisha baadae aliachiwa huru baada ya agizo lililotolewa na Rais Magufuli kupitia  Mwakyembe ambapo aliomba aonane na Nay wa Mitego ili kumshauri vitu vya kuongeza kwenye wimbo wake wa ‘WAPO’.

Full video tayari nimekuwekea hapa chini….

MillardAyo

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364