-->

Shilole Apanga Makubwa Kwenye 40 ya Mtoto wa Nuh Mziwanda

Shilole aka Shishi Trump ni mzungu. Amesema hana kinyongo na ex wake Nuh Mziwanda na ndio maana mwaliko wa 40 ya mtoto wa kike wa Nuh na mke wake Nawal ukihusika, ataenda kufanya makubwa.

Shiole akiwa na Nuh Mziwanda

“Mimi sinaga shobo ujue,” muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio hivi karibuni.

“Mimi naenda kwa moyo wangu kwamba ntaenda kama msanii mwenzangu kwamba hongera kwa kupata mtoto vizawadi hivi kama vibeseni, si unajua tena mama yake mkubwa wa zamani lazima naye.. sina tatizo,” aliongeza.

Nuh Mziwanda akiwa na mke wake

Alipoulizwa kwanini hakumpa mtoto Nuh kwenye uhusiano wao, staa huyo alijibu, ‘hatukujaaliwa tu.’ Shilole amesisitiza kuwa bado yupo single kwa sasa.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364