-->

VIDEO: Uwoya afungukia Kutoka na Harmorapa

Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hajawahi kutoka kimapenzi na Harmorapa na wala hajawahi kukutana na msanii huyo bali amekuwa akimsikia tu akifananishwa na Harmonize na hajawahi hata kukutana naye.

Akiongea kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachoruswa mubashara kila siku ya Jumatano kwenye ukurasa wa facebook wa EATV, Irene Uwoya amesema amekuwa akiona picha zake zikiwa zimeunganishwa na huyo msanii kwenye mitandao ya jamii huku wakisema kuwa wapo pamoja.

“Unajua tangu nimesema napenda watu wenye muonekano wa kiume ndiyo nimekuwa naona watu wakiunganisha picha zangu na huyo Harmorapa, lakini ukweli ni kwamba sijawahi hata kuonana naye live, wala kuongea naye kwa simu, ila namsikia tu watu wakimfananisha na msanii mwingine”. Alisema Irene Uwoya

Pia amezungumzia tetesi za kuwahi kutoka kimapenzi na msanii wa bongo fleva, Diamond Platnumz, ambapo amesema kuwa hajawahi kutoka naye, na kwamba kama kuna mtu anayedai jambo hilo kutoka, lazima awe ni mtu ambaye alikuwepo eneo la tukio.

bali na hilo Irene Uwoya amekataa kata kata tetesi za kuwa anatoka kimapenzi na msanii Dogo Janja kutoka Tip Top Connection na kusema yeye anamuona Dogo Janja ni kama mtoto wake, sababu ni mdogo sana na kusema anamuheshimu kama msanii mwenzake na kupenda kazi zake lakini hatoki naye kimapenzi.

Irene Uwoya alizidi kueleza kuwa kwa sasa hafikirii kuwa na mtu mwingine yoyote na kusema yeye anampenda sana mume wake Ndikumana na kusema yeye hajaachana na mume wake kama ambavyo watu wamekuwa wakisema.

“Mimi sijaachana na Ndikumana kwani sijawahi kupewa talaka ila nampenda sana mume wangu, saizi tuko mbali kwa sababu mimi niko busy na kazi na yeye yupo busy na kazi, kwa hiyo saizi nipo single sababu nampenda mume wangu” alisisitiza Irene Uwoya

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364