-->

VIDEO: Wasanii Tupunguze Bata – Riyama

Msanii wa filamu nchini Riyama Ally amefunguka na kutoa sababu kubwa zilizopelekea tasnia ya movie nchini kushuka kuwa ni pamoja na wasanii kudharau wamashabiki zao, kupuuza maoni ya watazamaji na kufanya vitu visivyoendana na jamii.

Riyama Ally

Riyama alisema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live na na kuongeza kwamba ukiacha dharau ambazo mastaa wamekuwa wakionyesha kwa mashabiki zao  sababu nyingine ni pamoja na wasanii kuendekeza starehe sana.

Hata hivyo Riyama amewataka wasanii hao kujipanga upya, kuwa wamoja na kuwaheshimu mashabiki ambao wamewafanya kuwa hapo walipo na kusema wasiendeshwe tu na watu kwa maslahi yao binafsi.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364