-->

VIDEO: Wastara Aibukia Kwenye Bongo Fleva

Msanii nyota wa filamu Tanzania Wastara ameanza kufanya muziki na tayari ameanza kuandaa albam yake.

eNewz ya EATV imemshuhudia msanii huyo wa bongo movie akiwa anafanya video yake ya kwanza aliyowaimbia wanawake na kusema kuwa tayari ameshakamilisha albam yake ambayo ndani ya mwezi huu atakuwa ame’shoot’ video 3 kwa mpigo, na albam itakamilika mwezi Juni mwaka huu.

Pia amesema show yake ya kwanza ataifanyia Sweden tarehe 18 mwezi huu kwenye kongamano la wanawake kutoka bara la Afrika ambapo yeye amechaguliwa kuiwakilisha Tanzania.

“Baada ya kutoa speech yangu kwenye kongamano hilo nchini Sweden, usiku nitaingia kufanya show maalum ambayo ilitolewa nafasi kwa mwanamke wa kitanzania, kwa bahati nzuri nikapata bahati na siendi kwa ajili ya kuimba tu bali na kuzungumza na wanawake ambapo kutakuwa na nchi zaidi ya ishirini……Baada ya nyimbo hii nitashoot nchini Sweden halafu kuna video kama tatu pia nitashoot Sweden halafu nitamalizia hapa Tanzania” Amesema Wastara

Msikilize hapa Wastara ambaye ameanza kwa kulitoa ufafanuzi sakata la mpenzi wake bondi, kukamatwa kwa tuhuma za ujambazi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364