-->

VIDEO:Wasanii Huu ni Wakati wa Kupendana-Johari

STAA wa filamu nchini, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kuwa kwa sasa wasanii wa maigizo wanapaswa kushikamana na kuondoa tofauti zao.

Blandina Chagula ‘Johari’

Johari ameyasema hayo leo wakati akipiga stori na mwandishi wetu akiwa katika Makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya sala fupi ya kumwombea aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba aliyefariki siku kama ya leo Aprili 7, 2012.

Akimwelezea Kanumba katika kumkumbuka, Johari amesema:

“Kila mwaka lazima nimkumbuke  Steven Kanumba kwani ndiye alikuwa akinitia faraja na nguvu ya kutokata tamaa katika jambo unaloliamini.

“Kanumba hakupenda kushindwa kwa kile alichokiamini, hakika pengo lake halitazibika, namwombea huko aliko alale mahali pema peponi, alipigania tasnia ya filamu, sema ndiyo hivyo hakuweza kufikia malengo yake, siwezi kumsahau, nitamkumbuka kwa mengi aliyoniachia.”

Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012, nyumbani kwake, Vatcan-Sinza jijini Dar ambapo aliyekuwa mpenzi wake kwa siri, staa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alihusishwa na kifo hicho. Mpaka sasa ni miaka mitano imepita.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364