Wahyda Mkwe wa Mr Blue Atoboa Haya Kuhusu Kugombana na Mr Blue
Mke wa msanii wa Hip hop bongo Mr. Blue Bi. Wahida maarufu kwa jina la Wahida wa Mr. Blue, ametoa sababu ambayo iliwafanya yeye na mumewe kupigana mara kwa mara.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Wahda amesema wakati wanamlea mtoto wao wa kwanza wa kiume Heri Samir, walikuwa na changamoto kubwa kwani alikuwa halali usiku kwa kulia, ndipo walipokuwa wanagombana mpaka kupigana na Mr. Blue ili kupokezana kumbembeleza mtoto.
“Kila mtoto anakuja kivyake, kama Heri alikuwa anapenda sana kukesha usiku, Heri tumekesha nae miezi 9 ndiyo kaja kuanza kulala usiku yani ikifika saa 12 ndiyo analala, ikifika usiku kuanzia saa 6 yuko macho mpaka asubuhi, tulikuwa tunapigana sana na baba yake, baba yake anataka kulala huku mtoto analia, tunapokezana tumemlea mpaka miezi 9 ndiyo akaanza kulala vizuri”, alisema Wahida.
Wahida aliendelea kwa kusema kuwa hali hiyo haikujitokeza kwa mtoto wao wa pili wa kike, hivyo walikuwa na wakati mzuri kumlea.
Wahida na Mr. Blue wana watoto wawili mmoja wa kiume mwenye miaka mitano, na wakike anatarajiwa kutimiza miaka miwili mwezi wa 10 mwaka huu.
EATV.TV