Wakonta Apata Kifaa cha Kumsaidia Kuandika
MWANDISHI wa ‘script’ anayetumia ulimi kuandikia, Wakonta Kapunda, amepata kifaa cha kumsaidia kuandika kwa kutumia sauti ambacho ndiyo ameanza kukifanyia mazoezi.
Wakonta aliliambia MTANZANIA kwamba kupatikana kwa chombo hicho kiitwacho Nuance Dragon Naturally Speaking, kitamrahisishia kuandika kwa haraka script za filamu zake na mambo mbalimbali ambayo atataka kuyafanya.
“Kupatikana kwa kifaa hicho ni faraja kwangu kwasababu ninachotaka kukiandika nazungumza kupitia kipaza sauti chake kisha chenyewe kinaandika katika kompyuta,” alisema Wakonta huku akifurahia kifaa hicho.
Kifaa hicho kimetolewa na msamaria mwema, Olivia Soko ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Whirl Market Technologies kutoka Afrika Kusini aliyeguswa na hali ya mwandishi huyo kutokana na ajali aliyopata siku ya mahafali yake ya kidato cha sita miaka minne iliyopita na kumsababisha kupooza kuanzia shingoni kushuka chini.
Mtanzania