Wamehamia kwa Kajala na Shetta
UBUYU wa leo unawahusu mastaa wawili Kajala Masanja na Shetta kudaiwa kuwa ni wapenzi huku ikielezwa wanatumia mbinu ya danganya toto kwa kitendo cha Shetta kuonyesha ukaribu kwa mtoto wa Kajala anayeitwa Paula.
Ziliwahi kuzagaa habari kuwa Shetta na Paula ni wapenzi lakini Shetta alipinga taarifa hizo na kusema kuwa anampenda mke wake na hawezi kumsaliti tena kwa mtoto mdogo kama Paula wa Kajala.
Hata hivyo, kwa sasa habari zimegeuka na madai mapya ya kudai Shetta ni mpenzi wa kajala na wanafanya siri kwa kulinda ndoa ya shetta.
Mwanaspoti liliongea na Kajala na kusema, Shetta ni mshikaji wake na kwamba watu wametoka kuzusha kwa mwanae na sasa wameamua kumvaa yeye.
“Kweli huu Ubuyu wa Shetta unazunguka tu katika familia yangu, watu washahama kwa mwanangu wamehamia kwangu duu, sio kweli bana Shetta ni mshikaji wangu sana,” alisema Kajala.
Mwanaspoti