-->

Wasanii Bongo Muvi Wachangia Damu Palestina

1.Mkongwe wa maigizo, Ahmed Olotu 'Mzee Chilo'akishiriki zoezi la kuchangia damu.Anayemuhudumia ni muuguzi wa Hospitali ya Parestina. Mkongwe wa filamu, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’akishiriki zoezi la kuchangia damu. Anayemuhudumia ni muuguzi wa Hospitali ya Palestina.2.Wakishiriki zoezi la kuchangia damu. Mzee Chilo na Bakari Makuka wakiwa tayari wanatolewa damu.3. Wasanii wakiongozwa na Davina na Koletha wakiwa kwenye tukio hilo Baadhi ya wasanii wa filamu wakisubiri kuchangia damu katika Hospitali ya Sinza Palestina.4.Msanii,Elizabeth Kilili akiandaliwa kutoa damu na muuguzi wa Hospitali ya Sinza. Msanii, Elizabeth Kilili akiandaliwa kutoa damu na muuguzi wa Hospitali ya Sinza.5.Ummy Mohammed akishiriki kuchangia damu hospitalini hapo. Mmoja wa wasanii waliojitokeza kwenye uchangiaji huo, Ummy Mohammed akiwa kwenye zoezi la kuchangia damu.6.Ummy (kulia) akipata ushauri kabla ya uchangiaji damu. Ummy (kulia) akipata ushauri kabla ya uchangiaji damu.7. 8.Wasani wa kuigiza waliojitokeza hospitalini hapo wakiwa katika tabasamu. 9. 10

Wasanii wa filamu waliojitokeza hospitalini hapo wakiwa katika tabasamu.

WASANII wa filamu hapa nchini leo wamejitokeza kuchangia damu pamoja na kufanya usafi Hospitali ya Sinza ’ Palestina’ kwa hiari ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli.

Katika zoezi hilo wasanii mbalimbali wa filamu walifika katika hospitali hiyo kutekeleza agizo la kufanya usafi ambapo mkongwe wa filamu nchini, Ahmed Olotu ’Mzee Chilo’ alikuwa mmoja wapo.

Akizungumza na wanahabari hospitani hapo, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Ally Mohammed ‘Baucha’ alisema kuwa lengo lao ni kuonyesha juhudi za kumuunga mkono Rais Magufuli alilowataka Watanzania wote kufanya usafi kila wiki ya mwisho ya mwezi pia kusafisha mazingira yao yaliyopo katika jamii.

Amesema pia wao kama wasanii wanahaki ya kusaidia akina mama wajawazito wanaopoteza maisha wakijifungua kwa kuwa na uhitaji muhimu wa damu na kuongeza damu wagonjwa wenye mahitaji muhimu.

‘’Niwaombe Watanzania wengine wawe mfano kutoka kwetu katika kushiriki uchangiaji damu kwani hospitali nyingi hazina damu yakujitosheleza kukidhi mahitaji ya wagonjwa” alisema.

Stori: Denis Mtima na Gladnes Malya/Gpl

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364