-->

Wasanii Hatupendani: Aisha Bui

Msanii wa bongo movie nchini Aisha Bui amefunguka na kusema kuwa bongo movie haitaweza kuendelea kama wasanii wenyewe hawatapendana na kushirikiana wenyewe.

aisha-bui

Akiongea na eNewz, amesema kuwa kama wasanii hawatakuwa na upendo wowote basi hata kazi zao za sanaa bado hazitaweza kufanikiwa.

“Wasanii tuwe na upendo na tuwe na ushirikiano, sisi wenyewe tuwe na upendo kwa sababu tumeshaichukulia kama kazi na tunalipa kodi serikali kupitia hizo hizo filamu kwa hiyo mimi naomba serikali pia iangalie kuhusu hili swala la movie hapa kwetu nchini’ alisema Aisha Bui.

Aidha kuhusu wasanii kutumia kiki katika kazi zao naye alisema kuwa kwa upande wake yeye anaona kama kiki hazisaidii kabisa.

“Mimi ninavyoona kiki hazisaidii kabisa ila ukitaka kujua hizi kiki hazina faida uliza mashabiki na hilo nimeona mara nyingi kutokana na skendo ila mimi ninachoamini ni kwamba kazi yako ikiwa nzuri pia watu watakukubali”

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364