-->

Wasanii Wanamkimbia Marco Chali – Master Jay

Mtayarishaji mkongwe wa muziki na mmiliki wa studio ya ‘Mj Records’ Master J amefunguka na kusema kuwa ukimya wa ‘Producer’ Marco Chali kwenye muziki unatokana na wasanii wengi kuogopa gharama zake.

Master-J

Master Jay alisema haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa wasanii wamekuwa wakiwakimbia watayarishaji wa muziki ambao wameweka misimamo yao kwenye gharama za utengenezaji wa muziki.

“Mimi nilishakaa na Marco Chali nilimuuliza juu ya hatma ya maisha yake, maana anaweza kuwa anafanya kazi na kazi zinasikika sana lakini yeye hapati maslahi, hivyo toka alipobadili malipo ya utengenezaji wa kazi wasanii wakakimbia, hivyo saizi yeye ameweka kiwango chake ukitaka kufanya naye kazi, hivyo wasanii wanakimbia na kwenda kwa watayarishaji wengine ambao wanatengeneza muziki kwa bei ya chini. Siyo Marko Chali tu saizi hata Lucci toka ameweka kiwango chake anachohitaji kufanya kazi wasanii wamemkimbia anafanya matangazo tu” alisema Master Jay

Mbali na hilo Master Jay anasema kuwa watayarishaji wengi wa muziki hivi sasa bongo hawapo vizuri kiuchumi ukilinganisha na wasanii kutokana na ukweli kwamba maproducer hao hawana msimamo, hawana umoja hivyo wasanii wanakuwa wanawatumia.

“Unajua hili suala siwezi kuwalaumu wasanii kwani wao ni wafanya biashara wanataka faida lakini ukweli ni kwamba sisi maproducer hatuna msimamo, hatuna umoja ndiyo maana wasanii wanatutumia wanavyotaka, maana wewe ukiweka bei ya juu wanakwenda kwa mwingine ambaye atatengeneza ngoma zao kwa bei ya chini, hivyo unakuta msanii ana maisha mazuri lakini producers wana maisha ya chini sana” alisema Master Jay

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364