-->

JB Kuja na Surprise ya Kalambati Lobo Septemba

MWIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya filamu Swahilihood Jacob Stephen ‘JB’ anatarajia kuja na Surprise kubwa pale atakapoachia filamu kubwa na y a kipekee ya Kalambati Lobo, akiongea na FC mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahilihood amefunguka kwa kusema kuwa awali alikuwa akiamini kuwa atatumia muda mwingi kuigiza tu bila kutayarisha sinema lakini kwa sasa amekua.

jb06

“Kuna wakati haikuwa rahisi sana kumwamini msanii chipukizi kwa ajili ya kuwapa kazi waigize wao bila mimi kuwepo lakini baada ya kufanya vizuri katika filamu ya Bado Natafuta na Chausiku nimewaamini chipukizi wakiwezeshwa wanaweza,”alisema JB

“Nina surprise kubwa sana nitakapoachia filamu yangu ya Kalambati Lobo kutoka kwa kampuni yangu mwenyewe ya Jerusalem Film Company nataka kuwaachia vijana wafanye kazi na niwasimamie,”

jbee

Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii msanii huyo amekuwa akiposti kuhusu kuachana na kazi ya uigizaji na kufanya kazi nyingine ili aweze kufanya kazi tofauti na kuigiza yeye mwenyewe bali kuwa mtayarishaji mkuu wa filamu Bongo.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364